AZAM FC KAMILI KUWAVAA SIMBA

Kikosi cha waoka mikate wa Chamazi Azam FC,kwa sasa kipo vizuri kwa ajili ya kukabiliana na Simba hapo kesho katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya FA,mchezo utakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,msemaji wa Azam fc,Jafari Idd alisema kwamba wachezaji wote wako vizuri na kwa pamoja wameshiriki mazoezi hata kwa wale ambao walikuwa majeruhi.

Alisema kwamba kumekuwa na maswali mengi yanayolenga kujua juu ya uwezekano wa nahodha wao John Boko kucheza kwenye pambano hilo,ambapo Jafari ameeleza kuwa mchezaji huyo anaweza kucheza endapo atakuwa kwenye mipango ya kocha mkuu.

No comments