ZAIDI YA WANACHAMA 925 WAJITOKEZA KUICHANGIA YANGA

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba zoezi la uchangiaji timu toka kwa wanachama linaenda vizuri ambapo kwa siku ya jana pekee takribani wanachama 925 wamejitokeza kuchangia zoezi hilo.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga alisema kwamba uongozi utakuwa ukitoa taarifa ya makusanyo kwa wanachama wake kila baada ya wiki moja ili waweze kufahamu mwenendo wa michango yao kwa klabu.

Kwanza nisema nawashukuru wote wale ambao wamechangia na wanaondelea kuchangia kuna wengine wamechanga mara mbili kwa kiasi kikubwa na sisi tutaangalia namna ya kuwasapoti kidogo nafikiri taarifa kamili tutaitoa tukapopanga siku ya kuwathamini"alisema Mkwasa.

No comments