KAMBI YA MOROGORO YAWAPA MATUMAINI SIMBA

Kikosi cha timu ya soka ya Simba kinaendelea vizuri na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao la nusu fainali ya kwanza ya kombe la FA dhidi ya Azam Fc mchezo ambao unataraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi.

Mratibu wa Simba,Abasi Ally alisema kwamba kikosi hicho kimeweka kambi mkoani Morogoro tangu siku ya juzi kwa dhamira ya kufanya vyema kwenye mpambano huo.

Abasi alisema kwamba wachezaji wote wako vizuri na anaamini wataibuka na ushindi mbele ya Azam FC kwani mara nyingi huwa wanakuwa na rekodi nzuri wanapokutana na timu hiyo katika mechi mbalimbali.

Katika hatua nyingine Abasi alisema kwamba licha ya kupokwa pointi tatu walizopewa awali na kamati ya saa 27 kwa upande wao hawana wasiwasi na jambo hilo kwani wanaamini nia yao ya kuchukuwa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara iko palepale.

Alisema kwamba wanachofanya kwa sasa ni kushinda mechi zao tatu ambazo zimesali na hawataangalia nani kafanya nini kwani wanaamini hata mpinzani wao Yanga anaewafukizia huenda akapoteza baadhi ya mechi na ikawa nafuu kwa upande wao.

No comments