JANG'OMBE BOYS YAICHAKAZA TAIFA JANG'OMBE



NA SULEIMAN USSI, ZANZIBAR.
Timu ya Taifa  Jan’gombe imekubali kipigo cha 1-0 dhidi ya watani wao Jan’gombe boys katika mchezo ambao ulipigwa katika uwanja wa Amani hapo jana majira ya saa 2 za usiku kwa saa za hapa nyumbani.

Nimchezo wa ligi kuu ya Zanzibar ambapo timu zote zilionekana kucheza kwa kasi katika kipindi cha kwanza lakini hakukuleta matunda yoyote katika kipindi cha hiko kwa timu zote.

Kipindi cha pili timu zote zilirudi uwanjani kwa kasi zaidi lakin timu ya Taifa ya Jan’gombe ilipunguzwa kasi baada ya mchezaji wao mmoja Ally  Kani kupingwa kadi nyekundu katika dk ya 50

Licha ya kadi hiyo  Taifa ya Jan’gombe walionekana kucheza kwa umakini wa hali ya juu  huku Jang’gombe Boys wakionekana kupata mwanya mzuri wa kuwashambulia lango la wapinzani wao ambapo mashambulizi hayo yaliisaidia Jan’gombe Boys kupata bao la ushindi lililofungwa na mchezaji  Khamis Mussa  (raisi)  katika dk ya 86.

Bao hilo lilidumu hadi dakika 90 ya mchezo na kupelekea timu ya Jong'ombe Boys kuzoa alama zote tatu kwenye pambano hilo lililowakutanisha mahasimu wa jadi visiwani Zanzibar.

No comments