TANZANIA PRISONS WAJIPANGA KWENYE MECHI ZA LIGI KUU
Kocha mkuu wa timu ya Tanzania Prisons Abdalah Mohamed amesema kwamba baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la FA katika hatua ya robo fainali na kikosi cha Yanga,kwa sasa nguvu zao wanazielekeza mwenye michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.
Mohamed alisema kwamba kikosi chake kimefungwa kihalali kwenye pambano la jana lililopigwa kwenye uwanja wa taifa kwani wapinzani wao Yanga walitumia nafasi zao tatu vizur ambao kwao walifanya makosa.
"Tushaondolewa huku kwenye FA sasa tunarejea kwenye ligi,hivyo dhamira yetu ni kushinda mechi zote ambazo zimesalia ili tukae sehemu nzuri kwenye msimamo wa ligi"alisema Mohamed.
Katika mchezo wa jana Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Prisons kwenye mchezo huo wa robo fainali ya mwisho kupitia kwa wachezaji wake Amisi Tambwe,Obrey Chirwa na Simon Msuva.
Droo ya FA ya timu zitakazocheza nusu fainali itapangwa leo hii ambapo timu zilizofanikiwa kuingia hatua hiyo ni pamoja na Azam FC,Mbao FC,Yanga pamoja na Simba.

Post a Comment