YANGA YAZINDUA RASMI ZOEZI LA KUICHANGIA TIMU

Klabu ya Yanga leo hii imezindua rasmi utaratibu wa wanachama na mashabiki kuichangia pesa timu ili kuongeza mapato ya klabu kutokana na kulegalega kwa hali ya uchumi ndani ya klabu hiyo.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charse Boniphace Mkwasa alisema kwamba uongozi wa klabu hiyo umeingia makubaliano maalumu na kampuni ya Selcom ili wanachama na mashabiki wapate fursa ya kuichangia timu yao.

"Ni ombi la wanachama wenyewe kujitolea kuichangia timu yao na sisi kama uongozi tumeona ni jambo lenye tija,hii haina tafasiri ya kwamba klabu haina fedha na imekwama kabisa kujiendesha bali tumelipitisha ili kukidhi matakwa ya wengi"alisema Mkwasa.

Kwa mujibu wa Mkwasa  namba ya kuichangia klabu kwa kutumia mtandao wowote wa simu ni 150334 ambapo jina litatokea YOUNG AFRICANS SPORT CLUB.

No comments