SIMBA YAPOKWA POINTI TATU ZA MEZANI

Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji imezirejesha pointi tatu kwa klabu ya Kagera Sugar baada ya kamati hiyo kubaini kuwa kamati ya saa  72 ya TFF ilitenda kosa kuipoka pointi tatu klabu ya Kagera Sugar.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa TFF,Selestine Mwesigwa alisema kwamba kamati imebaini kuwa rufaa ya klabu ya Simba iliwasilishwa nje ya muda ambapo ni kinyume na kanuni za uendeshaji wa mpira wa miguu.

Hata hivyo Mwesigwa alisema kwamba kuna baadhi ya viongozi wa kamati ya saa 72 ya TFF watapelekwa katika kamati ya nidhamu na maadili kwa mahojiano zaidi baada ya kubaini kuwa viongozi hao waliipotosha kamati ya usimamizi wa ligi.

No comments