TFF YAMTIA PINGU YA MWAKA MMOJA HAJI MANARA

Kamati ya maadili ya TFF imemfungia mkuu wa mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara kutojihusisha na mpira wa miguu kwa muda wa miezi 12 sawa na mwaka mmoja pamoja na kupigwa faini ya shilingi milioni 9.

Uamuzi huo umetolewa baada ya kamati hiyo kubaini kuwa Manara alitenda kosa siku ya jumatano katika mkutano na waandishi wa Habari kwa kutoa kauli ambazo kimaslahi haziendani na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu hapa nchini.

No comments