WAAMUZI WA MECHI YA KAGERA SUGAR NA AFRIKA LYON KUJADILIWA

Kufuatia kuwepo kwa taarifa za waamuzi ambao walichezesha mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Afrika Lyon na Kagera Sugar kutofautiana na kuipa kazi kubwa kamati ya TFF katika utoaji wa maamuzi wa rufaa iliyowasilishwa na vilabu viwili vya Simba na Kagera Sugar,leo hii uongozi wa kamati ya waamuzi umeweka bayana juu ya swala hilo.

Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ya TFF,Salum Umande Chama alisema kwamba kwa upande wao kama uongozi unasubiri taarifa rasmi kutoka kwa kamati hizo ili kubaini mapungufu yaliyojitokeza kwa upande wa waamuzi hao juu ya swala la kadi tatu za njano zinazodaiwa kuwa nazo mchezaji Mohamed Fakh

Chama alisema baada ya kupitia taarifa hizo endapo kama watabaini kuwa waamuzi hao wamefanya uzembe hawatasita kuwachukulia hatua za kisheria kwa kwenda kinyume na kanuni za waamuzi.

No comments