MJUMBE YANGA AWAPA SIMBA SIKU SABA KUTOA USHAHIDI

Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Yanga aliyesimamishwa katika mkutano mkuu wa zarura uliotishwa na mwenyekiti wa klabu ya Yanga,Salum Mkemi ameseshangazwa na hatua za baadhi ya taarifa ambazo zinaenezwa na wapinzani wao kuwa klabu ya Yanga inahusika kununua mechi za ligi kwa ajili ya kupata ushindi.

Mkemi amesema kwamba uongozi wa klabu hiyo unakemea jambo hilo na kwa sasa wametoa siku saba kwa hao wahusika wa jambo hilo kutoa ushahidi wao.

Amesema kwamba endapo kama watashindwa kufanya hivyo kwa upande wao wamejipanga kikamilifu kulifikisha swala hilo katika vyombo vya dora ili kupata suruhisho kamili.

Hata hivyo amedai kuwa kauli hizo zinazotolewa na wapinzani zina lengo la kuwaogopesha waamuzi wanaochezesha mechi za Yanga kuwa waoga ili washindwe kufuata sheria 17 za soka pindi timu hiyo inapokuwa uwanjani.

No comments