KAMATI YA MASAA 72 YAPEWA JUKUMU LA KUTOA MAAMUZI JUU YA MCHEZO KATI YA YANGA NA MBEYA CITY

Baada ya mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Mbeya City uliochezwa siku ya jana kutawaliwa na vurugu kwa upande wa wachezaji wa timu hizo,Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,Limewataka wadau wa soka hapa nchini kuwa na subra juu ya kutaka kufahamu kile ambacho shirikisho kitaamua.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba kwa sasa kwa upande wao wanasubiri lipoti kutoka kwa kamishina wa mchezo huo uliomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 pamoja na waamuzi kabla ya kamati ya masaa 72 kutoa maamuzi yake.

"Nawaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subra juu ya jambo hilo kwani kwa sasa TFF hatuwezi kuzungumza chochote hadi hapo tutakapota lipoti kutoka kwa wahusika ambao nadhani leo hii zitafika hapa TFF"alisema Lucas.

Amesema kwamba siku ya leo wanataraji kupata taarifa hizo na baada ya hapo kamati husika itakaa kuzipitia lipoti na ndipo kamati itatoa majibu kama kutakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.

No comments