MTIBWA SUGAR WAWAPONGEZA KINA SHIZA RAMADHANI KICHUYA

Uongozi wa timu ya Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro kupitia kwa msemaji wake Kifaru umewapongeza wachezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar ambao kwa sasa wanakipiga katika vilabu vya Simba na Yanga baada ya kuonyesha kiwango kikubwa na kuwa msada kwa timu zao.

 Kifaru amesema kwamba mbali ya kuwa msemaji wa klabu hiyo lakini amekuwa akiwapa ushauri mzuri wachezji hao akiwemo Shiza Ramadhani Kichuya,Mohamed Ibrahim,Mzamiru Yasini ambao wanaitumikia vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba pamoja na Andrew Vicenti na Hassani Ramadhani Kessy ambao wanaitumikia timu ya soka ya Yanga.

Amesema kwamba kufanya vizuri kwa wachezaji huo kumetokana na malezi bora ya uongozi wa Mtibwa Sugar kwani kwa muda wote uongozi umekuwa masada mkubwa kwao kuwapa mafunzo mazuri.

Hata hivyo Kifaru amesema kwamba Mtibwa Sugar ni chuo cha soka chenye malezi bora hivyo wanaamini licha ya kuondokewa na idadi kubwa ya wachezaji lakini wana matumaini ya kuzalisha wachezaji wapya ambao watakua bora zaidi.

No comments