GEITA GOLD NA POLISI TABORA NDIO BASI TENA KUCHEZA LIGI

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba halitapitia upya hoja ya timu ya Polisi Tabora pamoja na Geita gold kwa kuwa klabu hizo zimeshindwa kufuata taratibu na kanini za TFF.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba klabu hizo licha kuwasilisha hoja zake lakini kwa upande wao hawatakaa kwa mara nyingine kujadili jambo hilo kwa kuwa zimeshindwa kufuata utaratibu wa kanuni ikiwemo kufanya usajili kwa njia ya mtandao.

Lucas amesema kwamba TFF hawawezi kujadili hoja hizo kwani endapo kama hoja zitajadiliwa na timu hizo zikashinda kesi zao kutakuwa na kazi kubwa kwao kwani klabu hizo zitakuwa hazina hata mchezaji atakaepaswa kucheza ligi.

No comments