YANGA WAKANUSHA TAARIFA ZA MANJI KUJIUZULU

Uongozi wa Yanga umesema kwamba unasikitishwa sana na ujumbe unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ukidai kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yussuph Manji amejiuzulu.

Uongozi unawaomba wanachama wote kuupuzia ujumbe huo maana ni uongo na hakuna jambo kama hilo toka kwa mwenyekiti wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa ujumbe ambao umekuwa ukisambaa kwenye mitandao ulisomeka kwamba Manji amejiuzulu katika klabu ya Yanga baada ya serikali kusitisha mpango wa ukodishwaji,hivyo ameamua kujiuzulu huku akisisitiza kuwa klabu inapaswa kulipa deni ambalo klabu hiyo inadaiwa ya bilioni 12 baada ya ongezeko.

No comments