SAKATA LA HASANI KESSY SIMBA NA YANGA SASA WAANZA KUPATA MUAFAKA

Swala mchezji Hassani Ramadhani Kessy bado halijapatiwa ufumbuzi licha viongozi wa timu hiyo hapo jana kuweza kukutana.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba swala hilo licha ya kutopatiwa ufumbuzi kwa siku ya jana lakini viongozi wa timu hiyo wameonyesha kuelewana wao wenyewe pasipo kuwepo na msuluhishi yeyote.

Lucas amesema kwamba pande hizo hapo jana zilikutana pasipo kuwepo msuluhishi wa jambo hilo na wenyewe kwa pamoja wameridhiana kukaa tena siku nyingine sehemu watakayoipanga ili kulimaliza jambo hilo.

Amesema kwamba uongozi wa klabu ya Simba ambao uliwasilishwa na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakharia Hans Pope umefikia hatua ya kupunguza kiasi cha fedha kwa asilimia kumi kuhusiana na madai ya awali ya dola laki sita ambapo kiasi kwa sasa zinafikia shilingi milioni 200 za Tanzania.

No comments