LICHA YA BMT KUSTISHA MFUMO WA MABADILIKO,TFF WADAI HAWAJAPATA BARUA
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba bado hawajapokea baraua kutoka katika baraza la michezo la taifa BMT kuhusiana na taarifa yake ya ustishwaji wa mfumo wa mabadiliko yanayotakiwa kufanywa na vilabu vya Simba na Yanga.
Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba ingawa bado hawajapokea barua hiyo kwa ajili ya kuziwasilisha kwa vilabu husika lakini kama wao wasimamizi wa mpira wa miguu wanaendelea kuheshimu maamuzi hayo ya serikali.
Juma lililopita katibu mkuu wa BMT Mohamed Kiganja alisema kwamba baraza hilo limestisha mfumo wa hisa na ukodishwaji kwa vila vya Simba na Yanga kwa kuwa vilabu hivyo havijafuata taratibu za katiba zao,hivyo wanatakiwa kusitisha hadi hapo watakapoanza kufuata taratibu za sheria na katiba zao.
Post a Comment