MBAO FC WAPO KAMILI KUWAVAA KAGERA SUGAR

Uongozi wa klabu ya Mbao FC ya Ilemela jijini Mwanza umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuwakabili Kagera Sugar hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.

Msemaji wa timu hiyo Christiani Malinzi amesema kwamba mara baada ya kukamilika kwa mechi yao dhidi ya Yanga kwa sasa kikosi kimerejea jijini Mwanza kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao la kesho pamoja na mchezo wao wa siku ya jumapili dhidi ya Azam FC.

Christian amesema kwamba kwa sasa kocha mkuu wa klabu hiyo anaendelea kuyafanyia kazi mapungufu ambayo yamejitokeza katika michezo yao iliyopita ili wafanikiwa kupata matokeo mazuri.

Hata hivyo amewataka mashabiki wa Mbao kujitokeza kwa wingi hapo kesho ili kutoa hamasa ya kutosha kwani mshabiki ni mchezaji wa 12.

No comments