MAGUFULI ACHUKIZWA NA MASHABIKI WANAONG'OA VITI

Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema kwamba yeye ni mmoja kati ya wanaopenda michezo lakini hapendi kuona baadhi ya michezo inatawaliwa na vurugu.

Magufuli ameyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na wahariri wa vyombo Habari Ikulu leo hii ambapo amedai kwamba vurugu zinazofanywa na mashabiki zinaleta athari kwa taifa mfano mzuri swala la ung'oaji wa viti katika uwanja wa Taifa.

Amesema kwamba kuna kipindi alidiliki kwenda kutizama mechi za mchangani kuliko kushuhudia mechi kubwa  kama ya Simba na Yanga ambao mashabiki wao wanafanya vurugu zisizo na msingi ikiwemo kung'oa viti.

Hata hivyo amesema kwamba sababu hizo ndizo zinamfanya yeye kushindwa kujitokeza viwanjani kushuhudia mechi mbalimbali.

No comments