MZEE KINESI ASEMA SIMBA ITAPATA USHINDI WA 2-0 MBELE YA YANGA

Aliyewai kua makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba,Joseph Itang'ale maarufu mzee Kinesi amesema kwamba kikosi cha timu ya Simba kitachomoza na ushindi wa mabao 2-0 mbele ya watani wao wa jadi Yanga hapo siku ya jumamosi katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Itang'ale amesema kwamba sababu kubwa inayopa chachu ya kusema hivyo ni ushirikiano uliopo kwa sasa ndani ya timu hiyo kutoka kwa wachezaji,viongozi na mashabiki ambapo tangu kuanza kwa ligi wamekua pamoja.

Amesema kwamba ingawa msimu uliopita hawakufanikiwa kupata matokeo mazuri ya ushindi mbele ya Yanga hasa baada ya kufungwa mechi mbili lakini matokeo hayo hayateleta tija ya kuzuia ushindi kwa wekundu hao wa msimbazi.

No comments