JESHI LA POLISI LATOA RAI KWA MASHABIKI KATIKA MECHI YA KESHO YA SIMBA NA YANGA

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Saimon Siro amesema kwamba kwa upande wao kama jeshi la Polisi hapa nchini wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa siku ya mchezo huo hakutatokea uvunjifu wa Amani.

Siro amesema kwamba katika kuhakikisha mchezo huo wa kesho unachezwa kwa usalama wamejipanga kuweka askari wa kutosha kila pembe ya uwanja ili kuwadhibiti wale ambao watakua na nia mbaya, hivyo amewataka wadau wa mpira wa miguu kama kuna mtu anataraji kwenda kufanya vurugu uwanjani ni vyema akabaki nyumbani.

Amesema kwamba kwanza mashabiki ni vyema wakafahamu kua barabara inayopitia uwanja wa Taifa itafungwa na hatoruhusiwa mtu yeyote kuingia na chupa za maji, kinywaji chochote ama kifaa kitakachohatarisha uvunjifu wa amani uwanjani hapo.

"Magari ya washawasha yatakua ya kutosha askari wa jeshi la polisi pamoja vyombo mbalimbali watakuwa wengi zaidi hivyo yule ambae atakua na nia mbaya ni vyema akabaki nyumbani"alisema Siro.

No comments