KUELEKEA MECHI DHIDI YA YANGA SIMBA WAFICHA KAMBI YA TIMU HIYO

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba kwa sasa hawako tayari kuufahamisha umma ilipo kambi ya timu hiyo hasab kuelekea kwenye pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Yanga hapo siku ya jumamosi.

Meneja wa Simba,Mussa Hassani Mgosi ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba kambi ya timu hiyo itabaki kua siri kwani hawatapenda kuona kila mmoja anafahamu ilipo kambi hiyo.

"Tangu kuanza maandalizi yetu ya msimu huu kumekua hakuna utaratibu wa kutangaza kambi pale tunapokua na mechi ya ligi labda nikuulize wewe Said lini ulifahamu ilipo kambi ya Simba?kwa hiyo naomba wanachama watuelewe hivyo hatuko tayari kuwafahamisha kambi ilipo"alisema Mgosi.

Amesema kwamba sababu kubwa  ya kufanya hivyo ni kuwazuia wapinzani wao ili wasipate nafasi ya kufahamu mbinu zao kabla ya mechi husika.

Aidha amesema kwamba maandalizi kwa ujumla yanaenda vizuri na wana matumaini makubwa ya kuifunga Yanga katika pambano hilo kwani wana kikosi kizuri na chenye uwezo wa kupambana wakiwa uwanjani.

No comments