WACHEZAJI WA FRIENDS NI WAZEMBE,UONGOZI WAKILI KUSHINDWA KUIENDESHA TIMU

Baada ya kufungwa na timu ya Mshikamano kwa jumla ya mabao 5-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza,leo hii uongozi wa klabu ya Friends Rengers ya jijini Dar es salaam umesema kwamba sababu kubwa ya kufungwa kwao ni uzembe wa wachezaji kushindwa kujitambua.

Meneja wa timu hiyo Shabani Masilah amesema kwamba wachezaji wa timu hiyo kwa asilimia kubwa wamechangia timu kupata matokeo mabaya kwani wengi wao wamekua hawafanyi mazoezi kwa wakati husika.

Amesema kwamba mbali na wachezaji kuwa wazembe lakini sababu nyingine kubwa ambayo inawafanya kushindwa kuiendesha timu ni ukata wa kifedha kwani timu haina wafadhili.

Katika hatua nyingine Masila amesema kwamba kwa sasa uongozi  uko tayari kuiuza timu hiyo kwa kua hawana uwezo wa kuiendesha timu bila ya wadhamini.

Amesema kwamba kwa sasa wana mpango wa kufanya mazungumzo na Daimond pamoja na mkuu wa wilaya ya Ubungo ili wawasaidie kwenye jambo hilo kwani Friends Rengers ni timu ya wanachama na hao ambao wamewalenga ni miongoni mwa wahusika wakuu wa timui hiyo.

No comments