AFRIKA SPORT WAANZA SAFARI YA KUIFUATA ASHANTI UNITED

Msafara wa wachezaji 20 na viongozi watano wa timu ya Afrika Sport ya mkoani Tanga ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza leo hii umeelekea jijini Dar es salaam tayari kwa kujiiwinda na pambano lao litakalopigwa siku ya jumatatu kwenye uwanja wa Karume dhidi ya Ashanti United.

Meneja wa timu hiyo Nurdini Gogola amesema kwamba maandalizi kwa upande wao yamekamilika na mechi hiyo wanaipa umuhimu mkubwa kwani ndio itakayoanza kuwapa taswira ya kurejea katika ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

Amesema kwamba wanaamini wanataraji kupata ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao kwani Ashanti ni moja ya timu zenye uzoefu wa michuano mbalimbali ikiwemo kuwai kucheza ligi kuu lakini jambo hilo halikuwa kikwazo kwa upande wao kutopata pointi tatu muhimu.

No comments