TFF YATANGAZA VIINGILIO VYA MECHI YA YANGA NA SIMBA




Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF limetangaza iingilio vya mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba mchezo unaotaraji kupigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,Ofsa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kwamba kiingilio cha chini ni shilingi elfu saba kwa viti vya rangi ya kijani,bluu na najano huku kiingilio cha juu kikiwa shilingi elfu 30.

Lucas amesema kwamba ni vyema watanzani wapenda soka wakaanza kununua mapema tiketi hizo zinazotaraji kuanza kuuzwa hapo kesho sehemu mbalimbali kwa njia ya mtandao.



Nae meneja miradi wa kampuni ya Celcom ambayo ndio imepewa jukumu la kuratibu uuzaji wa tiketi kwa njia ya mtandao Gallus Runyeta amesema kwamba kwa upande wao wamejipanga kikamilifu kuhakikisha hakutakua na kasoro zozote ambazo zitajitokeza katika pambano hilo.

Amesema kwamba katika kuhakikisha kua wanaondoa usufu kwa watakaotaka kuingia uwanjani wameamua kupanga utaratibu wa kuuza tiketi kila pembe ya eneo kupitia mawakala wake.

Runyeta amewataka pia mashabiki wafanye haraka kununua mapema tiketi zao kwani tiketi zitakapoisha hakutakua na njia mbadara ya mtu kuingia uwanjani.




No comments