BAADA YA KUWA MAFICHONI SIMBA YAREJEA JIJINI DAR ES SALAAM

Baada ya kua mafichoni kwa ajili ya kambi ya kujiwinda na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Yanga hapo kesho katika pambano linalotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba kikosi cha timu hiyo tayari kimerejea jijini Dar es salaam leo hii.

Makam wa Raisi wa klabu hiyo Godfrey Nyange Kaburu amesema kwamba tayari kikosi kimeshatua jijini Dar es salaam na wachezaji wote wapo vizuri kwa ajili ya pambano linalovuta hisia za wapenda soka.

Amesema kwamba kwa upande wao wamejipanga kikamilifu kuelekea kwenye mchezo huo na wana matumaini makubwa ya kuchomoza na ushindi hjasa kutokana na morali iliyopo kwa wachezaji,viongozi pamoja na mashabiki.

"Kiukweli kwa sasa tuko vizuri mwenyewe si unaona kasi iliyopo kwa sasa kwa hiyo tusubiri tu mechi hiyo ya kesho na naamini tutawafunga Yanga"alisema Kaburu

No comments