MOHAMED DEWJI AWAJAZA NOTI WACHEZAJI NA VIONGOZI WA SIMBA


Uongozi wa klabu ya Simba umemshukuru mlezi wa klabu hiyo ambae pia ametangaza nia ya kutaka kununua hisa za 51 za klabu hiyo Mohamed Dewji kwa kuanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika uongozi wa Simba zinasema kwamba  Dewji maarufu kama MO tayari ameshaanza kulipa mishahara ya wachezaji,benchi la ufundi na Sekretarieti ya klabu na atafanya hivyo katika kipindi chote cha mpito kuelekea kwenye mabadiliko ya kimuundo ya klabu.

Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka kwa uongozi wa Simba zinasema kwamba mbali na hayo  mfanyabiashara huyo mkubwa barani Afrika atalipia kodi za nyasi bandia na gharama nyingine za uendeshaji.

Hata hivyo uongozi wa Simba unashukuru kwa jambo hilo hii inatokana na klabu hiyo kwa sasa kutokua na mdhamini ambae klabu ingeyumba endapo Dewji asingeyafanya haya kwa sasa ndani ya klabu hiyo yenye makazi yake mitaa ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaam.

No comments