YANGA YAELEKEA PEMBA KUJIWINDA NA PAMBANO LAO DHIDI YA SIMBA

Kikosi cha timu ya Yanga leo hii kimeelekea kisiwani Pemba kikitokea mkoani Shinyanga kwa ajili ya kujiandaa na pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Simba hapo siku ya jumamosi katika mechi inayotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Baada ya mechi ya jana dhidi ya Stend United iliyopigwa mkoani Shinyanga na Yanga kufungwa kwa bao 1-0 leo hii alfajili kikosi kilianza safari ya kwenda Mwanza ambako walipanda ndege iliyowapeleka Pemba.

Kaimu katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Baraka Deusidedit ingawa hakupenda kuweka bayana juu ya kambi hiyo lakini ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kua kikosi kipo Pemba na taarifa rasmi za kambi hiyo zitapatikana kwenye mitandao yao pindi uongozi utakapokua tayari kuzungumzia jambo hilo.

Amesema kwamba kwa upande wao kama viongozi wa klabu hiyo wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa wanapata matokeo mazuri kwenye mechi hiyo dhidi ya Simba kwani ni mchezo wa kawaida na hawana hofu juu ya hilo.

"Nisingependa sana kuzungumza juu ya kambi ilipo maana wakati ukifika taarifa zitawekwa kwenye mitandao ya klabu lakini fahamu timu haipo Shinyanga wala Mwanza lkn kuelekea kwenye pambano hilo tumejipanga vizuri na kila kitu kipo safi"alisema Baraka.

Hata hivyo Baraka amedai kua matokeo ya jana ya kufungwa na Stend United hayawapi hofu yeyote kwani mpira ni mchezo wa makosa hivyo benchi la ufundi litayafanyia kazi mapungufu ambayo yameonekana.

No comments