VICTOR COSTA AWATAKA VIONGOZI WA SIMBA KUTOWADHARAU YANGA

Mchezaji wa zamani wa Simba,Victor Costa amesema kwamba pambano kati ya Yanga na Simba ni gumu na timu yeyote inayo nafasi ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia mishale ya saa kumi kamili jioni kwa saa za hapa nyumbani.

Costa pia amewatahadharisha viongozi wa Simba kuwa wasibweteke na matokeo ambayo wameyapata katika michezo ya ligi kuu au kuwazarau wapinzani wao baada ya kufungwa na Stend United kwani siku zote mechi hizo hua na matokeo tofauti na matarajio ya watu wengi.

"Mimi nawashauri viongozi wa Simba na wanachama wa klabu hiyo wasilete mzaha kwa wapinzani wao kwani Yanga ni nzuri na ina wachezaji wenye vipaji hivyo wanaweza kubadilisha matokeo wakati wowote"alisema Costa.

Simba na Yanga zinataraji kumenyana siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa na pambano hilo kwa sasa limekua gumzo kila kona ya mtaa huku kila upande ukijinasibu kufanya vizuri.

No comments