MANJI AKABIDHI EKARI 715 KWA AJILI YA UJENZI WA UWANJA

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Mehboob Manji ameipa klabu hiyo eneo la ekari 715 lililopo Geza Ulole Kigamboni jijini Dar es salaam kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu pamoja na kituo cha kukuzia vipaji vya wana michezo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba na maofsa wa chama na Serikali ya Kigamboni.

Akipokea eneo hilo kwa niaba ya kalbu mwenyekiti wa baraza la wadhamini  wa klabu hiyo mama Fatuma Karume amesema kwamba sasa rasmi ujenzi utafanyika katika eneo hilo lililobatizwa jina kijiji cha Yanga SC.


No comments