KALLY ONGALA AREJEA RASMI MAJIMAJI

Klabu ya Majimaji ya mkoani Ruvuma imekamilisha mpango wake wa kumrejesha kocha wa zamani wa timu hiyo Kally Ongala mara baada ya hii kumpa kandarasi ya mwaka mmoja kwa ajili ya kuwafundisha wanalizombe hao wa Songea.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,Ongala amethibitisha kurejea kwake ndani ya timu hiyo na ameahidi kuiongoza vyema timu hiyo ili iepukane na janga la kushuka daraja.

Amesema kwamba anaamini atakua kwenye mazingira magumu ya ufundishaji ndani ya timu hiyo hasa mara baada ya kupoteza mechi 6 mfululizo lkn atahakikisha atapambana vya kutosha kuona Majimaji inafanya vizuri katika michezo ambayo imesalia.

No comments