RAIS WA FIFA AHUDHURIA MKUTANO WA CAF
Rais wa Shirikisho la soka duniani
FIFA Gianni Infantino, yupo jijini Cairo nchini Misri anakohudhuria mkutano
usiokuwa wa kawaida wa Shrikisho la soka barani Afrika CAF.
Mkutano huo unaongozwa na Issa
Hayatou rais wa CAF, pamoja na viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika.
Ajenda kuu ya mkutano huu ni
kuwachagua watu wawili watakao keti katika Baraza kuu la FIFA.
Ongezeko la watu hao wawili
litafikisha idadi ya uwakilishi wa bara Afrika katika Baraza hilo kufikia
wajumbe saba kutoka watano.
Wanaowania nafasi hizo mbili ni pamoja na Ahmad (Madagascar), Almamy Kabele Camara (Guinea),
Djibrilla Hima Hamidou (Niger), Kwesi Nyantakyi (Ghana) na Augustin
Senghor (Senegal).
CAF imekuwa ikiwakilishwa katika
Baraza hilo la FIFA na Issa Hayatou, Lydia Nsekera kutoka Burundi, Tarek
Bouchamaoui kutoka Tunisia, Constant Omari kutoka DRC na Fatma Samoura kutoka
Senegal pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo.
Post a Comment