SERIKALI YAKABIDHIWA UWANJA WA TAIFA WA UHURU


Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhiwa rasmi uwanja wa Taifa wa uhuru uliopo jijini Dar es salaam leo hii baada ya ukarabati uliofanywa na kampuni kutoka nchini China [BCEG] kukamilisha zoezi hilo.

Akipokea uwanja huo kwa niaba ya Serikali,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye amewapongeza wakandarasi kutoka China ambao wamefanikiwa kujenga kiwanja bora ambacho kina hadhi ya kimataifa.

Nape amewataka watanzani ambao watapa fursa ya kuutumia uwanja huo wautunze vizuri kwa maendeleo ya Taifa ili kiwanja kiendelee kua na ubora

Aidha amesema kwamba ni vyema ada ambazo zinapaswa kulipwa kwenye uwanja huo zikalipwa kwa uhalisia ili zitumike kwenye maboresho ya uwanja huo ambao unataraji kuanza kutumika kwa baadhi ya mechi za ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments