MANJI AMREJESHA BIN KLEB YANGA KATIKA KAMATI YA MASHINDANO

Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji ameunda Kamati mpya ya mashindano na kuvunja rasmi kamati ya mashindano ambayo ilikua chini ya Isaac Chanji aliyejiuzulu nafasi hiyo mwezi mei mwaka huu.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii kaimu katibu mkuu wa klabu hiyo Baraka Deus Dedit amesema kwamba mwenyekiti amevunja rasmi kamati ya mashindano na kuunda kamati mpya baada ya kua na mamlaka ya kuteua wajumbe watatu kikatiba na pia kutengua uteuzi na kuunda kamati kwa mujibu wa katiba ya Yanga.

Amesema kwamba kamati hiyo itaongozwa na mwandisi Paul Malume na mwandisi Isac Chanji atabaki kua mshauri wa kamati hiyo ya mashindano.

WAJUMBE WENGINE WA KAMATI HIYO NI

Musa Ulungo,Mahende Mugaya, Abdalah Bin Kleb, Jackson Maag, Samwel Lukumay,Hussein Nyika, Athumani Kihamia kutoka Arusha,Felix Felician Minde kutoka Mwanza, Leornad  Chinganga Bugomola kutoka Geita,Omary Chuma,Hussein Ndama,Hamad Ally Islam kutoka Morogoro,Yusuphexl Mhaden,Beda Tindwa,Moses Katabalo, Roger Lamlembe na John Mogha kutoka Mbeya.

 

No comments