YANGA YAKAMILISHA RATIBA KWA KUFUNGWA NA TP MAZEMBE
Timu yasoka ya Yanga imekamilisha ratiba katika ushiriki wa michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya TP MAZEMBE kwenye mchezo uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Stade de TP Mazembe nchini Congo.
TP Mazembe imefanikiwa kupata ushindi huo kupitia kwa wachezaji wake Jonathan Boling pamoja na Rashifod Kalaba huku bao la kufutia machozi kwa Yanga likifungwa na mchezaji Amisi Tambwe kunako dk ya 75.
Katika mchezo huo mchezji Endrew Vicente Dante amelimwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea mazambi mchezaji wa timu ya TP Mazembe.
Kwa matoke hayo Yanga imemaliza michuano hiyo ikiwa katika nafasi ya mwisho mwa kundi A wakiwa na alama 4 huku TP Mazembe wakiongoza kundi hilo wakiwa na pointi 13.
TP Mazembe imefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika huku timu nyingine itakayoungana na TP Mazembe itajulika hapo baadae kati ya Mo Bejaia wenye alama 5 na Medeama ya Ghana yenye alama 8 ambapo kwa sasa timu hizo zipo uwanjani zikicheza mechi ya mwisho itakayoamua mshindi.
Post a Comment