MGOSI ATAMBA SIMBA ITAENDELA KUPATA USHINDI HAPO KESHO


Wakati ligi kuu ya Tanzania bara ikitaraji kuendelea kutimua vumbi hapo kesho kwenye viwanja tofauti hapa nchini, Meneja wa timu ya Simba Musa Hassani Mgosi amesema kwamba wanaamini watafanya vizuri katika mchezo wao wa hapo kesho wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya timu ya JKT Ruvu ya mkoani Pwani.

Mgosi amesema kwamba wachezaji wote wapo vizuri ispokua mchezaji Hamadi Juma ndio hayupo kambini kutokana na kusumbuliwa na majeraha baada ya kuanguka bafuni na kupasuka kichogoni.

Amesema kwamba wanaamini pambano la kesho linataraji kua na ushindani mkubwa kwani wapinzani wao wapo vizuri na wanaifahamu vyema ligi ya Tanzania bara.


No comments