PORTO,MONACO,CELTIC ZA FUZU HATUA YA MAKUNDI KLABU BINGWA ULAYA


Klabu ya Celtic ya nchini Scotaland imefanikiwa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, baada ya kutinga kwenye nafasi hiyo kwa tofauti ya bao la ugenini dhidi ya klabu ya Hapoel Beer Sheva.

Ikikubali kichapo cha mabao 2-0 ilipokuwa ugenini nchini Israel, kikosi cha kocha Brendan Rodgers, hata hivyo kimefanikiwa kutinga hatua ya makundi ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu.
Celtic sasa inafuzu kwa faida ya bao la ugenini kwa kupata ushindi wa jumla ya mabao 5-2.
Katika mechi nyingine, klabu ya Italia ya AS Roma yenyewe ilishindwa kufuzu kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa Ulaya, baada ya kushuhudia wachezaji wake wawili wakitolewa nje kwa kadi nyekundu na kukubali kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya FC Porto ya Ureno.
AS Roma ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutinga kwenye hatua ya makundi kufuatia sare ya bao 1-1 kwenye mechi ya awali, lakini mara baada ya bao la mapema la mchezaji Felipe, klabu hiyo ilichanganyikiwa na kuruhusu mabao zaidi
Wachezaji Daniele de Rossi na Emerson Palmieri ndio waliokuwwa wa hanga wa mwamuzi wa kati baada ya kuoneshwa kadi nyekundu zilizoigharimu timu yao.
Roma iliyokuwa iwe timu ya tatu kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa Ulaya, sasa inaachia nafasi hiyo kwa vinara wa Italia, Juventus na Napoli ambao wamo kwenye droo itakayochezeshwa Alhamisi ya Agosti 25.
Katika mtanange mwingine, klabu ya Dundalk ilishindwa kuwa timu ya kwanza kutoka Ireland kufuzu kwenye hatua ya makundi baada ya kushindwa kwa sheria ya bao la ugenini kwa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya Legia Warsaw ya Poland.
Monaco ya nchini Ufaransa, yenyewe ilifanikiwa kutinga kwenye hatua ya makundi baada ya kuwafunga Villarreal kwa bao 1-0, huku penalty ya mwisho iliyopigwa na mchezaji Fabinho ikitosha kuipa Monaco ushindi wa faida ya mabao ya ugenini kwa jumla ya magoli 3-1.
Klabu ya Bulgaria ya Ludogorets itaungana na Celtic, AS Roma, Legia Warsaw na Monaco kwenye hatua ya makundi baada ya kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya klabu ya Jamhuri ya Czech, Vicktoria Plzen na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2.

No comments