AZAM WAENDELEA KUZITAKA YANGA NA SIMBA ZICHEZE AZAM COMPLEX
Uongozi wa mabingwa wa ngao ya Hisani timu ya soka ya Azam
ya jijini Dar es salaam,umesema kwamba umepokea taarifa kutoka shirikisho la
mpira wa miguu hapa nchini TFF juu ya mpango wao wa kutaka mechi zao za ligi
kuu ya Tanzania bara ambazo watacheza na Yanga pamoja na Simba ziweze kuchezwa
kwenye uwanja wao wa Azam Complex.
Msemaji wa timu hiyo Jafari Idd amesema kwamba katika
taarifa yao ambayo wameipata kutoka TFF ni kwamba shirikisho hilo limekataa
mpango huo kwa sababu zilizoelezwa ni za kiusalama.
Jafary amesema kwamba anashangaa shirikisho hilo
kuwakatalia ombi lao ilihali uwanja wao una vigezo vyote ambavyo vimekamilika
sambamba na kupitishwa na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF juu ya
uwanja huo utumike kwenye mechi za mashindano.
Amesema kwamba sababu iliyotolewa na TFF haina mashiko
kwani jukumu la kiusala linapaswa kufanywa na jeshi la Polisi ambao wao ndio
wenye mamlaka juu ya jambo hilo.
Aidha uongozi wa klabu hiyo umesema kwamba utalitolea
ufafanuzi swala hilo pindi watakapomaliza mechi zao zijazo za ligi ikiwemo ya
Majimaji inayotaraji kupigwa siku ya jumamosi pamoja na mechi zinazofuata
watakazocheza mkoani Mbeya.
Post a Comment