MKWASA KUTANGAZA KIKOSI CHA WACHEZAJI 20 KESHO KWA AJILI YA MECHI DHIDI YA NIGERIA



Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,Charse Boniphace Mkwasa hapo kesho anataraji kutangaza kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Nigeria.

Msemaji wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba ingawa timu ya Taifa Stars haina nafasi ya kufuzu katika fainali za Afrika baada ya Misri kujihakikishia nafasi hiyo lkn mchezo huo ni muhimu kwani endapo kama Stars haitacheza itakumbana na adhabu kutoka CAF.

Amesema kwamba pia kocha mkuu ataitumia mechi hiyo kwa lengo la kukijenga kikosi hasa kifanye vizuri kwenye mashindano yajayo na kwa mujibu wa taarifa yake kikosi hicho atakutana nacho mara baada ya mechi za ligi kuu ya Tanzania bara zitakazopigwa tarehe 28 hadi 29 mwezi huu.

No comments