TFF YAJIPANGA KUIPELEKA KAMBINDI SERNGETI BOYS NJE YA NCHI,WAPINZANI WAO WASHITAKIWA KWA KUCHEZESHA VIJEBA



Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limesema kwamba lipo katika maandalizi ya kuiwezesha timu ya Serengeti Boys inakwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuweka kambai kabla ya kucheza mechi yao dhidi ya timu ya vijana ya Congo Brazavile ikiwa ni mikakati ya kusaka kucheza fainali za Afrika kwa vijana.

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba Raisi wa shirikisho mara nyingi amekua akitimiza ahadi zake ikiwemo swala zima la kuipeleka timu Madagasca kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na mechi yao iliyopita dhidi ya Afrika kusini ambapo kambi hiyo imekua na tija baada ya Serengeti Boys kusonga mbele kwenye mashindano kwa kufanikiwa kuwaondosha Afrika ya Kusini.

Lucas amesema kwamba wana Imani na kikosi cha timu hiyo kinachonolewa na kocha mkuu Bakali Shime kwani kinaonyesha mwanga katika ushiriki wao kwenye michuano hiyo pamoja na michezo mbalimbali.

Hata hivyo Lucas amesema kwamba huenda Serengeti Boys isicheze na Congo kwani kwa mujibu wa taarifa iliyopo ni kwamba timu ya vijana ya Namibia imekata rufaa wakidai timu ya vijana ya Congo imechezesha wachezaji ambao wamezidi umri.

No comments