JUMA MWAMBUSI ASEMA WAMEJIFUNZA MENGI KATIKA USHIRIKI WAO KATIKA MICHUANO YA KIMATAIFA


Baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika kwenye hatua ya makundi,kocha msaidizi wa timu ya Yanga,Juma Mwambusi amesema kwamba hatua ambayo imeishia timu hiyo ni hatua ya kupongezwa kwani kwa muda mrefu timu hiyo imeshindwa kupata nafasi kucheza hatua ya makundi.

Mwambusi amesema kwamba kupitia mashindano hayo wamefanikiwa kujifunza mengi ambayo watayafanyia kazi ili msimu ujao washiriki vyema kwani changamoto ambazo wamezipata ni elimu tosha kwao.

Amesema kwamba katika ushiriki wao kumekua na changamoto mbalimbali ikiwemo swala la kadi kwa wachezaji wao ambao limekua tatizo kwani baadhi yao walikosa mechi muhimu akiwemo Dornad Ngoma na Thabani Kamusoko na wachezaji wengine.

"Watanzania watambue mtoto huanza kutamba kisha hutembea pia msingi imara hujengwa kwa umakini mkubwa hivyo huu ndio muda tunaijenga timu kitaifa na kimataifa"alisema Mwambusi.

No comments