JAMALI KISONGO AWATAKA WATANZANIA WAIGE ANAYOYAFANYA SAMATA


Baada ya mchezaji Mbwana Samata kuisaidia timu yake ya KRC GENK kutinga kwenye hatua ya makundi ya michuano ya Europa kwa kufanikiwa kushinda bao moja katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Lokomotiva Zagreb ya Croatia,hii leo meneja wa mchezo huyo Jamali Kisongo amempongeza Samata kwa juhudi zake ambazo anaendelea kuzifanya akiwa nje ya nchi.

Kisongo amesema kwamba Samata ni mchezaji anaepaswa kuigwa na watanzania wengi kwani ni moja ya mchezaji anaetambua majukumu yake akiwa uwanjani na kufahamu nini ambacho anakifanya.

Amesema kwamba wachezaji wa wetu wa hapa nyumbani ni vyema wakaiga mazuri yake anayoyafanya ili kuleta tija hapa nchini juu ya maendeleo ya mpira wa miguu.

Katika hatua nyingine Kisongo amesema kwamba kwa sasa nchi mbalimbali kutoka nje ya nchi zimezidi kuelekeza nguvu zao hapa nyumbani kwa lengo la kupata wachezaji ambao watakwenda kucheza soka la kulipwa.

Kisongo amesema kwamba kwa sasa watanzania wanapaswa kuamini kua Tanzania ina idadi kubwa ya wachezaji bora lkn wanapaswa kuzingatia kua na nidhamu ya hali ya juu ndani ya uwanja na nje ya uwanja.

"Mfano mzuri ni Samata ambae amesajili kwa bei nafuu lkn kwa sasa ni mchezaji bora na ni muhimu tofauti na wachezaji wenzake ambao wamesajiliwa kwa fedha kubwa lkn hawafikii kiwango cha Samata"alisema Kisongo.

No comments