JUMA ABDULI AIPA YANGA UBINGWA

Na Said Ally
Beki wa kulia wa timu ya soka ya Yanga,Juma Abdul amesema kwamba kikosi cha timu yao kimejipanga vyema kuwakabili Stend United hapo kesho katika moja ya mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Abdul amesema kwamba kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya kuelekea kwenye pambano hilo ana imani Yanga itachomoza na ushindi.

Alisema kwamba kikosi chao kina nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao wa ligi hivyo ni vyema mashabiki na wanachama wakajitokeza kwa wingi kwenye pambano hilo ili kwenda kuwapa hamasa wachezaji.

No comments