WAMBURA AZUNGUMZIA MSIMU MPYA WA LIGI KUU

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniphace Wambura amesema kwamba mchakato wa maandalizi kwa ajili ya msimu huu wa ligi kuu ya Tanzania bara tayari ushaanza rasmi kwa bodi hiyo kupanga maswala mbalimbali ya utawala.

Wambura alisema kwamba kwa sasa bodi ya ligi imeshapata idadi ya viwanja ambavyo vitatumika katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara inayotaraji kuanza mwezi wa nane.

Alisema kwamba kwa sasa wanataraji kutuma wakaguzi kwa ajili ya kubaini ubora wa viwanja hivyo ili waanze kupanga ratiba ya michezo ya lig kuu ya Tanzania bara.

Aidha katika hatua nyingine Wambura alisema kwamba anaamini uongozi wake utazingitia matakwa ya vilabu ili kuondoa mvurugano wa ratiba ambapo mara nyingi kumekuwepo na lawama za baadhi ya vilabu na wadau wa soka juu ya upangaji wa ratiba.


No comments