NGOMA AZIKATAA SIMBA NA YANGA

Mshambuliaji wa timu ya Yanga Donald Ngoma ameachana rasmi na timu hiyo baada ya kusaini kandarasi ya miaka mitatu katika klabu ya Polokwane CIity ya nchini Afrika Kusini ambayo inashiriki ligi kuu.

Awali mchezaji huyo alikuwa anahusishwa kurejea hapa nyumbani siku ya kesho kwa ajili ya kufanya mazungumzo na klabu za Simba na Yanga ambapo Yanga ilikuwa na nia ya kumuongeza mkataba mpya huku nao Simba wakitaka kumsajili kwa ajili ya kukiimalisha kikosi chao.

Sasa baada ya Ngoma kusajiliwa na klabu hiyo kumesitisha tetesi ambazo zilikuwa zinaenea kwa kasi hapa nyumbani hasa wapi angeonekana msimu ujao kati ya Simba na Yanga.

No comments