TAMBWE AUNGANA NA DONALD NGOMA

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Yanga,Amis Tambwe ameongeza kandarasi ya miaka miwili kwa ajili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligu kuu ya Tanzania bara na michuano mingine.

Tambwe ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao ilikuwa inaelekea ukingoni ambapo uongozi umeamua kumpa kandarasi mpya baada ya kuridhishwa na kiwango chake.

Mchezaji huyo anaungana na Donald Ngoma pamoja na Mwinyi Haji ambao nao wameendelea kusalia kwa mabingwa hao wa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya wachezaji hao nao kuongeza mikataba.

No comments