TAKUKURU WASEMA HAYA KUHUSU KUWASHIKILIA MALINZI NA MWESIGWA

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imethibitisha kumshikiria Rais wa TFF,Jamali Malinzi na katibu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa kwa uchunguzi Zaidi.

Ofsa uhusiano wa TAKUKURU,Musa Misalaba amethibitisha jambo hilo akisema kwamba kwa sasa swala hilo lipo katika uchunguzi na kwa wakati huu hawawezi kuweka wazi hasa sababu za kushikiliwa kwao.

"Kiukweli ni kwa sasabu hili jambo ni la weledi si vizuri kuweka wazi kila jambao,lakini jambo la msingi unalotakiwa kuelewa ni kwamba ni kweli tunamshikilia tunaendelea na shughuli zetu za uchunguzi,lakini tumefikia wapi au tumefanya nini hilo swala ni la uchunguzi hatupaswi kuliweka wazi"alisema Misalaba.

Hata hivyo ameongeza kwa kusema kuwa swala hilo lisihusishwe na maswala ya uchaguzi mkuu wa TFF unaotaraji kufanyika agosti12 huko mkoani Dodoma kwani wao kwa muda mrefu walikuwa wanalifanyia kazi jambao hilo.

'Hili swala halihusiani na uchaguzi bwana wao waendelee tu na uchaguzi wao maana hili jambo halihusiani na swala hilo na sisi hatuwezi kuingilia uchaguzi kwani kila kitu kina taratibu zake"aliongeza Misalaba.


No comments