FIFA KUCHUNGUZA SWALA LA MALINZI

Viongozi wa shirikisho la soka duniani FIFA wanataraji kuwasili hapa nchini wikiendi hii kwa ajili ya kufuatilia swala zima linaloendelea hivi sasa linalohusiana na maswala ya Rushwa.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba viongozi hao watawasili hapa nchini kwa lengo moja tu la kufuatilia swala hilo linalohusiana na Rushwa.

Ujio huo unawasili hapa nchini baada ya viongozi wa ngazi ya juu wa shirikisho la soka hapa nchini TFF kushikiliwa na vyombo vya dora kwa tuhuma mbalimbali.

No comments