NGOMA AONGEZA MKATABA MPYA YANGA

Mshambuliaji wa timu ya Yanga Donald Ngoma leo hii ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kwa ajili kuendelea kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao.

Awali kulikuwepo na taarifa za mchezaji huyo kusajiliwa na klabu ya nchini Afrika ya Kusini baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali ambazo mitandao ya kimataifa iliripoti usajili wake wa kujiunga na klabu ya Polokwane City.

Mbali ya tetesi za kusajili na klabu hiyo lakini pia Ngoma alikuwa anahusishwa kusajiliwa na klabu ya Simba ambayo nayo kulikuwa na taarifa kuwa klabu hiyo ilikuwa inamuhitaji.

Hata hivyo baada ya leo hii  Ngoma kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu ya Yanga kunahitimisha uvumi uliokuwa unaenea katika sehemu mbalimbali.

No comments