SALUM MADADI ARITHI MIKOBA YA MWESIGWA

Kamati ya utenda ya TFF leo hii imekutana kwa ajili ya kujadili swala la uongozi,baada ya viongozi wa juu wa shirikisho hilo Rais na katibu wake kupatwa na matatizo.

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF,Salum Madadi alisema kwamba kamati hiyo imeadhimia kuteua baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo kukaimu nafasi zao hadi hapo kesi inayowakabili viongozi hao itakapomalizika.

Madadi alisema kwamba kamati imependekeza kuwa makamu wa Rais wa TFF,Wallace Karia kuanzia sasa abebe majukumu ya rais huku nafasi ya katibu ikaimiwe na yeye mwenyewe Salum Madadi.

Alisema kwamba kamati ya utendaji imeamua kufanya hivyo baada ya nafasi hizo kuwa sehemu muhimu ya utendaji wa kazi za TFF hivyo kukosekana kwa watu hao kungeleta athari kwa shirikisho.

No comments