MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI ATANGAZA KUJIUZULU

Kamati ya uchaguzi ya TFF inayoongozwa na wakili Revocuts Kuuli leo hii imeshindwa kupata muafaka juu ya zoezi la uchaguzi baada ya wajumbe wa kamati hiyo kutofautiana kwenye zoezi zima la usaili ambapo swala hilo sasa litatolewa ufafanuzi hapo kesho.

Mwenyekiti wa kamati hiyo wakili Revocutis Kuuli kwa upande wake ametishia kujiondoa kwenye kamati hiyo endapo wajumbe watakuwa na msimamo wao wa kua Rais Jamalinzi aendelee na mchakato wa kuwania uongozi pale tu atakapokuwa huru.

Kuuli alisema kwamba kamati hiyo imetofautiana kwenye swala zima la wagombea ambao wameshindwa kuwepo kwenye usaili hasa wale wanaoshikiliwa na vyombo vya dora ambapo wajumbe wa kamati hiyo wameshauri wagombea hao waendelee kuwepo kwenye mchakato wa uchaguzi licha ya kutokuwepo kwenye zoezi la usaili.

No comments